Ligi Kuu Tanzania Bara, inaendelea leo kwenye viwanaj tofauti nchini, huku vinara wa Ligi hiyo Simba leo wanashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu ili kuzidi kujikita kileleni wakati watawakaribisha Kagera Sugar.
Simba itakuwa kwenye Uwanja wa Uhuru huku Stand United wanaoshika
nafasi ya pili wakiwa wenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa CCM
Kambarage, Shinyanga.
Lakini kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amejihakikishia kuwatibulia Simba rekodi yao ya kutopoteza mechi kwa msimu huu toka uanze na kusema atanyamazisha tambo za mnyama .
Kagera ambayo ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 15 katika michezo tisa iliyocheza. Huku ikitaka ushindi kujihakikishia kukaa kwenye nafasi nzuri lakini Simba nayo itataka kuendelea kubaki kileleni hivyo mchezo unatarajiwa kuwa mkali baina ya timu hizo mbili. Kwani vinara hao wana pointi 20 katika michezo nane iliyocheza.
Kesho pia kutakuwa na mchezo utakaowakutanisha Yanga na Azam zote za jijini Dar, mchezo utakokuwa na hisia kali kutokana na muenendo mbovu kwa Azam.
Pia, Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya tano kwa pointi 14 nayo
itaendelea kusaka ushindi kwenye Uwanja wa Manungu dhidi ya Tanzania
Prisons ambayo nayo, haiko vizuri sana msimu huu, ukilinganisha na msimu
uliopita. Tanzania Prisons inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 10
katika michezo nane iliyocheza.
Timu zote mbili zinahitaji ushindi kwani atakayepoteza atakuwa kwenye
uwezekano wa kushuka kutoka nafasi moja hadi nyingine. JKT Ruvu na
Mwadui zitakutana zote zikiwa haziko katika nafasi nzuri.
Mwadui ina pointi nane katika michezo nane ikishika nafasi ya tatu
kutoka mwisho, na JKT Ruvu inashika nafasi ya nne kutoka mwisho ikiwa na
pointi nane sawa na Mwadui.
Kila mmoja anahitaji ushindi kujiondoa katika hatari ya kushuka
daraja. Vile vile, Majimaji ambayo inashika mkia itakuwa ugenini dhidi
ya Toto African kwenye uwanja wa CCM, Kirumba, Mwanza.
Timu hiyo ina pointi tatu ikishika nafasi ya mwisho, ikifuatiwa na
Toto inayoshika nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na pointi nane, wote
wakiwa wamecheza michezo tisa.

No comments:
Post a Comment