Saturday, October 15, 2016

CLYNE ASIFU UWEZO WA KLOPP LIVERPOOL.

Kloop akishangilia pamoja Clyne.
Nyota wa taifa la England Nathaniel Clyne anafurahia maisha chini ya kocha wa zamani wa Borrusia Dortmund Jurgen Kloop akiwa Liverpool.
Nyota huyo wa Liverpool anaamini kikosi chao kinaweza kila kitu na hakuna lisilowezekana kikiwa chini ya Klopp. alisema beki huyo wa Liverpool. 

''Amejenga kujiamini kwenye timu na kutufanya kuamini tunaweza kufanya lolote.

''Mfumo wake ndani ya timu unatufanya tuamini tunaweza kushinda kila mechi mbele yetu.'' Alisema Clyne. 

''Sisi wote tunafahamu kazi yetu ndani ya timu na anatusaidia hilo, na kila mtu anafurahia hilo.  
 

No comments:

Post a Comment