Sunday, September 11, 2016

GUARDIOLA- NILIMUANZISHA IHEANACHO KUONYESHA DHAMIRA YETU







 Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameweka bayana uamuzi wake wa kumuanzisha Kelechi Iheanacho kwenye mechi yao ya mahasimu kuwa ilikuwa ni ujumbe kwa wachezaji wake nia yao Old Ttafford.    


 Kinda huyo wa taifa la Nigeria amemzawadia kocha wake goli kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya United. Baada ya Sergio Aguero kusimamishwa, Guardiola amesema kuwa alikuwa na uchaguzi mwingine ambao alimchagua Iheanacho kuwaonyesha wachezaji wake nini anachohitaji.   


''Alikuwa ni streka pekee tuliekuwa nae kwa kipindi hiki,'' alisema kwenye mahojiano na Manchester Evening News, nilikuwa na mawazo mengi ya kuchagua lakini baadae nilifikiria kuwaonyesha wachezaji wangu kuwa tumekuja kushinda mchezo huu.''  


Pia aliongeza kuwa alipokea magoli mengi kutoka kwa vijana wa Mourniho kwenye counter-attack sababu United ni timu nzuri kwenye eneo hilo kwenye mchezo huo, sababu wana nguvu na warefu kuliko sisi lakini anashukuru kuwa waliweza kuwazuia. 

 


 

No comments:

Post a Comment