Sunday, September 11, 2016
BARCELONA YAPIGWA 2-1 NOU CAMP
Barcelona imekumbana na kipigo cha kwanza kwa msimi huu 2016/2017 kutoka kwa timu ya Deportivo Alaves cha 2-1 nyumbani kwao Nou Camp, huku MSN wakishindwa kupenya ngome ya wageni hao. Barcelona ambao walianza bila nyota wao Mesii na Suarez walioingia kipindi cha pili, Alaves walipata goli lao kwanza dakika ya 38 kupitia mchezaji wao Deyverson kabla ya kwenda mapumziko, na kipindi cha pili Barca walisawazisha kupitia Jeremy Mathieu dakika ya 46 lakini alikuwa Ibai Gomez aliepeleka kilio nyumbani kwa miamba hiyo ya Catalunya kwa bao lake la dakika ya 63 na kuondoka na pointi tatu Nou Camp.
Huku makamu wa Rais wa Barcelona Jordi Mestre akimtetea Neymar kuwa asingeweza kufanya lolote akiwa peke yake bila kuanza na wachezaji wenzake wanaojulikana kwa jina lao la MSN ambao walitoke benchi na kuingia kipindi cha pili cha mchezo huo.
Na sasa timu hiyo inajipanga kwa ajili ya mechi yake dhidi ya Celtic kwenye Champions League jumanne hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment