Baada ya hapo jana kuwa mmoja wa wafungaji wa Tottenham kwenye ushindi 4-0 dhidi ya Stoke City, Mchezaji wa timu ya Taifa ya England Harry Kane amefikisha magoli 50 katika ligi hiyo, huku akisema kuwa malengo yake ya kuwa na magoli 50 zaidi ndani ya klabu yake kwenye Premier League ndio yanaanza na ana matumaini ya kuwezekana haraka sana.
Mchezaji huyo alisema ''kwamba kwa miaka iliyopita kama mtu angeniambia kuwa unaweza kuwa na magoli 50 kwenye Premier League kwa Spurs basi ningechukulia kama ni furaha kabisa'', nitafanya kazi kwa bidii, na kujaribu kuendelea kufunga na kufanya hizo alama kuzidi kama sisi pamoja''.
Mchezaji huyo amefungua akaunti yake ya magoli kwa msimu kwenye mechi hiyo. Na imemchukua mechi 87 kuiletea mabao 50 ya ligi Spurs, na anataka kuwa bora zaidi kwa kufikisha mabao 100.
''Magoli 50 kwenye Premier League ni mafanikio makubwa sana kwangu na natumaini magoli 50 zaidi yatawezekana haraka sana.''
Hamna aliekuwa na mawazo kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kama angejitaidi zaidi na kutambulika White Lane Park hapo mwanzoni mwa kazi yake. Kane ambaye alivumilia kutolewa kwake kwa mkopo katika timu za Leyton Orient, Millwall, Norwich na Leicester hapo awali, kabla ya kupewa nafasi ya kuthibitisha uwezo wake katika klabu ya mzazi wake.
Kane alisema pia kuwa magoli yao yote yalikuwa ni magoli mazuri sana. Na alikuwa na furaha kwa kuifungia timu yake na kujiona bora mbele ya mashabiki wao.

No comments:
Post a Comment