Sunday, September 11, 2016

RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA SIERRA LEONE AMEACHIWA HURU


Baada ya Isha Johansen kukamatwa kama sehemu ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa na tume ya kupambana na rushwa nchini Sierra Leone ameachiwa huru.      
 

Tume hiyo ilimkamata  Johansen, mwanamke pekee duniani kuongoza Shirikisho la Soka, na maofisa wawili siku ya jumatano iliyopita.   


''Hii ilikuwa baada ya wao kushindwa kujibu ombi letu la mara kwa mara kutoa taarifa kwa sisi katika taarifa za matumizi ya fedha za Shirikisho hilo (SLFA),'' alisema kiongozi wa tume hiyo Ady Macauley.


''Nina furaha kuwaambia kuwa nimeachiwa bila mashtaka'' alisema Johansen kwenye barua yake aliyotia sahihi.   

''Kutokuwa kwangu na hatia katika madai yoyote yanayohusiana na rushwa au kosa lolote kuwa ni migogoro.''  

 

No comments:

Post a Comment