Tuesday, September 27, 2016

KASHFA YAMNG'OA ALLARDYCE ENGLAND

 


Baada ya kuitimikia England kwa siku 67 na kucheza mchezo mmoja tu kama kocha wa timu ya taifa ya England, Sam Allardyce
ameachana rasmi na kazi yake kama kocha wa England siku ya leo baada ya FA na bosi huyo wa zamani wa West Ham kufikiwa makubaliano ya pande zote mbili kusitisha mkataba.    
Allarydce mwenye umri wa miaka 61, ameingia kwenye kashfa iliyoibuliwa na gazeti moja nchini England ambapo inadaiwa alikutana na waandishi wa habari wa Daily Telegraph waliojifanya wafanyabiashara kutoka Mashariki ya Mbali ambao walihitaji ushauri juu ya uhamisho wa mabilion ya pound kwenye Ligi Kuu ''Premier League''.  

Wakati wa mkutano huo na waandishi hao waliojifanya wafanyabishara, Allardyce ameripotiwa kumkosoa mtangulizi wake Roy Hodgson akimaanisha yeye ''woy'' hana muonekano mzuri wa kuongea mbele ya uma.   

Bosi huyo wa zamani wa West Ham, Bolton Wanderers na Sunderland, alimrithi Roy Hodgson nafasi hiyo ya ukocha mwezi Julai mwaka huu.  

Na taarifa ya FA ilisema.

''Kwa mwenendo wa Allarydce, kama ilivyoripotiwa leo ilikuwa muafaka wa meneja wa England. Amekubali kuwa alifanya makosa makubwa ya hukumu hivyo anaomba radhi. Hivyo kutokana na mwenendo mbaya wa matendo yake, FA na Allardyce kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake. 

Huu sio uamuzi uliochukuliwa haraka, lakini kipaumbele cha FA ni kulinda maslahi mapana ya michezo na kudumisha viwango vya juu vya maadili katika soka. Meneja mwandamizi wa timu ya England ni nafasi ambayo lazima uonyeshe uongozi imara na kuonyesha heshima na uadilifu katika michezo wakati wote. 

Gareth Southgate anachukua nafasi hiyo kwa ajili ya mechi nne zijazo dhidi ya Malta, Slovenia, Scotland na Hispania, wakati FA ikiendelea kutafuta kocha mpya wa England. 

FA inamtakia Sam kila la kheri katika siku zake za baadae. 




No comments:

Post a Comment