Nyota wa Atletico Madrid Antoine Griezmann alihofia kuwa kocha wao Diego Simeone angejiunga na Paris Saint-Greman na mpango kufanyika miezi iliyopita.
Simeone alisababisha hali ya kutoelewana na klabu hiyo wakati akidai kufikiria mustakabali wake baada kupoteza fainali kwa penati kwenye Klabu Bingwa dhidi ya Real Madrid mwezi May.
Uvumi ulionyesha kwamba kiungo huyo wa zamani wa Argentina anaweza kuziba nafasi ya Laurent Blanc PSG, ingawa baadae alikubali mustabali wake na Atletico huku mabingwa wa Ligue 1 wakimchukua Unai Emery.
Griezmann ambaye alihusishwa na kujiunga na mabingwa hao wa Ufaransa kipindi cha usajili ameweka wazi kwamba Simeone alimwambia aendelee kubaki Atletico.
''Nilikuwa kwenye Michuano ya Euro, Ufaransa walikuwa wakisema kwamba mpango tayali umeshakamilika,'' Griezmann aliiambia Onda Cero pale alipouliza kuhusu tetesi za Simeone.
''Nilikuwa na hofu kwamba asingekuwepo hapa. Bado ninahitaji kufanya kazi na yeye, kujifunza kutoka kwake. Atletico wanamuhitaji.
''Aliniambia kuwa anabaki, na alizungumza na klabu na kila kitu kitakuwa sawa, mazungumzo hayo alinihakikishia uwepo wake.''
Griezzmann ambaye alikuwa na msimu uliopita Atletico, ambapo alifunga mabao 32 kwenye michuano yote, na sita na kutoa pasi kwenye timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye fainal za Euro 2016 na kumfanya kushinda kiatu cha dhahabu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 tayali ameshafunga mabao matano kwenye mechi za La liga kwa msimu huu na kuongeza kasi yake ya kuwa miongoni mwa wachezaji watatu wataochaguliwa kwa ajili ya tuzo ya Ballon d'Or, na amekubali kwamba kushinda tuzo hiyo itakuwa ni jambo muhimu kwake.
''Nahitaji kuendelea kukua na Atletico, klabu ambayo nitapata kufikia mambo makubwa,'' alisema. ''Ninajaribu kuwa bora na kufikia kiwango cha juu, kwa hiyo watu watasema kuwa mimi ni mmoja wachezaji wajuu.
''Lakini sihitaji wao wanifananishe na mtu au wengine, nahitaji watu wanijue kwa kuwa Griezmann.
''Itakuwa vizuri kwangu na wachezaji wenzangu kwenye klabu na Ufaransa , kushinda tuzo ya Ballon d'Or. Hata kama sitoipata, itamaanisha kwamba nahitaji kuendelea kufikia kiwango na kuendelea.

No comments:
Post a Comment