Tuesday, September 27, 2016

DORTMUND WALIMAANISHA WALICHOWAAMBIA MADRID JUU YA JEZI RANGI YA NJANO




Baada ya hapo jana Borrusia Dortmund kuwakejeli Real Madrid juu ya jezi za rangi za njano kuwa zinawapa tabu baada ya mfululizo wa droo na timu zilizovalia jezi rangi ya njano,
limethibitika leo hii kwenye mchezo wao  wa makundi kwenye Klabu Bingwa baada ya kutoka sare ya 2-2.


Huku Madrid wakiwa wa kwanza kufunga kupitia nyota wao Cristiano Ronaldo dakika ya 17 lakini ndani ya dakika 43 Aubamayeng alisawazisha bao hilo na kufanya kipindi cha kwanza kuisha kwa sare ya 1-1. Na ndani ya kipindi cha pili Varane alifunga bao la pili kwa Madrid dakika ya 68 ya mchezo na kujihakikishia kuondoka na pointi tatu ugenini hapo lakini alikuwa Schurrle aliepeleka maumivu kwa Madrid kwa bao lake la kusawazisha dakika ya 87, na kuthibitisha kauli yao juu ya jezi za njano kwa Madrid zinawapa homa ya manjano. 

Na kufanya mchezo huo uliochezwa Signal Iduna Park kumalizika kwa sare ya 2-2.

No comments:

Post a Comment