Sunday, September 4, 2016

VPL KUENDELEA LEO HII


Raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo Jumapili September 4, mwaka huu kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyotolewa  na Bodi ya Ligi (TBLB) ni kuwa kutakuwa na mchezo kati ya Stand united na Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.   

Ligi hiyo ambayo kwa sasa kimsimamo inaongozwa na Azam FC itaendelea jumatano kwa michezo mitatu ambako mabigwa watetezi Yanga Afrika watakaribishwa na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. 

Azam ambao wanaongoza ligi hiyo watasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine, huku Simba ikitarajia kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

''hapo jana tulishuhudia michezo mingine ya VPL ambapo Mwadui FC ilipoteza kwa wenyeji wao Kagera Sugar  kwa goli 1-0 ,na kufanya Kagera Sugar kufikisha pointi 5 katika michezo yao 3 waliocheza. Na katika mchezo mwingine wa VPL uliofanyika CCM Kirumba Mbeya City ilitoa kipigo cha 4-0 kwa wenyeji wao Mbao FC ya jijini humo. Huku JKT Ruvu na African Lyon zikitoka sare na timu ya Maji maji ikilala 1-2 kwa Mtibwa Sugar.
 

No comments:

Post a Comment