Saturday, September 3, 2016
TFF NA SEMINA KWA LIGI YA WANAWAKE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), limeandaa semina elekezi kwa klabu za ligi kuu za wanawake inayotarajiwa kuanza baadaye mwaka huu.Semina hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo,itafanyika jumamosi september 8,2016,kwenye Ukumbi wa Hostel za TFF zilizopo ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho hilo uwanja wa Kumbukumbu za Karume makutano ya barabara za Shauri moyo na Uhuru jijini Dar es salaam.
Ligi hiyo ya wanawake ni ya kwanza kufanyika nchini chini ya uongozi wa Rais Jamal Malinzi kwani kabla ya hapo hapakuwa na ligi inayohusisha mikoa mbalimbali . Shukrani za pekee ziende kwa kituo cha cha Televisheni cha Azam kilichoamua kudhamini ligi hiyo pamoja na ile ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
TFF imeandaa semina hiyo yenye lengo la kuwapa maelekezo kuhusu kanuni za ligi, usajili wa timu na taratibu nyingine za ligi hiyo ikiwemo ni pamoja na sheria za mpira wa miguu ambazo zimekuwa na marekebisho kwa msimu wa miguu 2016-2017 kama zilivyorekebishwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Timu zitazoshiriki katika ligi hiyo ni pamoja na Viva Queens ya Mtwara, Fair Play FC ya Tanga, Panama FC ya Iringa, Mlandizi Queens ya Pwani, Marsh Academy ya Mwanza, Baobao Queens ya Dodoma, Majengo Queens ya Singida, Kigoma Sisters FC ya KIgoma, Kagera Queens pamoja na Mburahati Queens, JKT Queens na Evergreen Queens za Dar es salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment