Wednesday, September 14, 2016

ZANZIBAR HOI TENA CECAFA





Timu ya taifa ya Mpira wa miguu wanawake ya Zanzibar hapo jana  iliendeleza mfululizo wake wa kufungwa kwenye michuano ya CECAFA Women's Champions  baada ya kuruhusu kufungwa na Uganda 9-0, timu hiyo ambayo ilipoteza dhidi ya Burundi kwa 10-1 kwenye michuano hiyo baada ya golikipa wao Amina Mohamed Kitambi kutolewa kwa kadi nyekundu na kufanya kucheza 10 uwanjani. Uganda ambao ni wenyeji wa michuano hiyo walipoteza mechi yao dhidi ya Kenya kwa 4-0 na kuzinduka kwenye mechi ya jana.   


Tanzania Kilimanjaro Queens ambao walipata ushindi kwenye mchezo wake dhidi ya Rwanda wa magoli 5-2 , Kocha wa Kilimanjaro Queens Sebastian Nkoma akihakikisha kwa timu yake kufanya vizuri kwenye mchezo wake unaofata dhidi ya Ethiopia Septemba 16, 2016.    
 
   

 

No comments:

Post a Comment