Maria Sharapova kufahamu hatima ya rufaa yake dhidi ya kupinga kufungiwa miaka 2 na Shirikisho la Kimatifa la Mchezo wa Tenisi (ITF )katika Mahakama ya Usuluhishi kwa ajili ya Michezo(CAS) mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Bingwa huyo mara tano wa Grand Slam alifungiwa na Shirikisho hilo baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni (Meldonium) kwenye michuano ya Australia Open mwaka huu.
''Mrussia huyo mwenye miaka 29, alisema kuwa amekuwa akitumia dawa hizo toka 2006 kwa ajili ya matatizo ya kiafya, alieleza kwenye rufaa yake ya kupinga adhabu hiyo.'' Alisema kuwa hakuwa na uchovu uliomfanya kutumia dawa hizo kuongeza nguvu kwenye michezo yake.
Meldonium zilipigwa marufuku kutumika mapema mwaka huu 1 January, 2016.
No comments:
Post a Comment