Wednesday, September 14, 2016

HATIMAYE UEFA IMEPATA RAIS MPYA LEO HII.

                                 Rais mpya wa UEFA Aleksander Ceferin kulia na Michael van Praag

Aleksander Ceferin amethibitishwa kuwa  Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Ulaya (UEFA) baada ya kumbwaga Michael van Praag kwenye uchaguzi uliofanyika leo Jumatano.  

Aleksandra ambaye alikuwa Rais wa Shirikisho la Soka Slovania (SFA), alionekana kama chaguo sahihi la kurithi nafasi iliyoachwa na Rais aliepita Michael Platin tokea mwanzo wa kura katika mkutano wa UEFA Anthens.         

Rais huyo mpya mwenye miaka 48 alipata kura 42 na kumpita mpinzani wake kwa kura 29 alizopata Michael van Praag ambaye alipata kura 13.   

''Marafiki wapenzi, ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu mzuri. Ni heshima kubwa lakini pia ni wakati wa majukumu makubwa.'' alisema Ceferin baada ya ushindi wake.   

''Nchi yangu ndogo ya Slovenia inajivunia ushindi huu, ahsanteni sana.'' 

Nafasi ya Rais wa UEFA ilikuwa wazi baada ya aliyekuwa Rais Michael Platin kujiuzulu nafasi yake baada ya kufungiwa kujihusisha na masuala ya mpira kwa miaka 4 kutoka 6 na Mahakama ya Usuluhishi kwenye Michezo kufuatia kuhusishwa kwenye malipo yasiyokuwa na maadili ya dola million 2 kutoka kwa aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter 2011.         

Ceferin sasa anachukua majukumu ya kiofisi yaliyoachwa na Platin mpaka kumaliizika kwa muhula wake 2019.  

Muslovenia huyo pia ametaka kuwepo na uwezekano wa mazungumzo juu ya Ligi ya Mabingwa kwamba Uingereza, Ujerumani, Italia na Hispania kuwa na uhakika wa matangazo 
manne katika Europe Premier Competition kuanzia 2018-2019.     

   


 

No comments:

Post a Comment