Toni Kroos akishangilia na wachezaji wenzake wa Real Madrid. |
Inakuwa ni habari njema kwa mashabiki wa Real Madrid duniani kote, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuthibitisha kwamba Toni Kroos amesaini mkataba mpya ambao unakuwa miaka sita na miamba hiyo ya Laliga baada ya kuongeza miaka miwili.
Kiungo huyo wa Ujerumani amejifunga na Los Blancos mpaka 2022 ambapo mkataba wake wa kwanza ulikuwa mpaka 2020 na hivyo kumfanya kumalizika msimu wa 2021/2022. Na mkataba huo unaogharimu Euro million 20 unamfanya kuwa mchezaji wa Kijerumani anaelipwa mshahara mkubwa kwenye historia ya soka.
Taarifa ya klabu hiyo ilieleza kuwa ''Real Madrid na Toni Kroos wamefikiana makubaliano ya kuongeza mkataba ambao utamuweka Madrid mpaka June 30, 2022.''
Kroos ambaye ameshaonekana Santiago Bernabeu kwenye mechi 108 toka ajiunge nao akitokea Bayern Munich mwaka 2014 kwA dau la Euro million 30.
Na kiungo huyo mwenye miaka 26 ameshashinda Kombe la Klabu ya Mabingwa, Kombe la Dunia la Klabu na UEFA Super Cups akiwa na klabu hiyo.
Huku kukiwa na taaifa kutoka nchini Uingereza kwamba Man U na Man City walikuwa wakijiandaa kupigania saini ya mchezaji huyo kwa msimu ujao.
No comments:
Post a Comment