Wednesday, October 12, 2016

YANGA YAIPIGA MTIBWA 3, SIMBA YAICHAKAZA MBEYA CITY KWAO.



 


Baada ya mfululizo wa matokeo mabaya kwenye mechi zao mbili zilizopita ikipoteza 1-0 dhidi ya Stand United na kupata sare ya 1-1 na mahasimu wao Simba SC, leo timu ya Yanga imeweza kurejesha matumaini ya kutetea taji lao la Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar ya Morogoro bao 3-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Klabu hiyo ya Jangwani ilijiptia bao lake la kwanza ndani ya kipindi cha kwanza likifungwa na Obrey Chirwa na kipindi cha pili walikamilisha kalamu yao ya mabao kupitia Msuva dakika ya 68 na Ngoma dakika ya 80, huku Haruna Chanongo akiifungia Mtibwa bao la kufutia machozi.






Huku mnyama akiondoka na pointi tatu Mkoani Mbeya kufuatia kuifunga timu ya Mbeya City ya mkoani humo, ambapo kabla ya mchezo huo timu hiyo ya Mbeya ilijitapa kukata ngebe za Simba kitu ambacho kimekuwa tofauti kwao kwa kuruhusu kipigo hicho nyumbani kwao kwenye Uwanja wa Sokoine. Mabao ya Kichuya na Hajib yaliweza kuizamisha Mbeya City nyumbani kwao.


Dakika sita ya mchezo Simba ilipata bao lake la kwanza kupitia Hajib na bao la pili Kichuya alifunga dakika ya 37 na kukata ngebe za Mbeya City.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuendelea kukaa kileleni mwa ligi kwa kufikisha pointi 20 kwa mechi nane zilizocheza.
 

No comments:

Post a Comment