Wednesday, October 12, 2016

UINGEREZA KUIKOSA EL-CLASICO DESEMBA 03 MWAKA HUU.

Barcelona's Lionel Messi shakes hands with Real Madrid's Cristiano Ronaldo before the game
Messi   na Ronaldo kwenye moja ya mechi yao ya El-Clasico LaLiga.


Desemba 03 mwaka huu kutakuwa na mechi ya kwanza ya mahasimu wa Ligi Kuu ya Hispania ''LaLiga'' Real Madrid dhidi ya Barcelona El-Clasico. Mchezo ambao huvuta hisia za watu wengi duniani kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizo  mbili za nchini Hispania.
Lakini ratiba ya Ligi hiyo dhidi ya mchezo huo haitakuwa rafiki nchini Uingereza kutokana na kutofautiana masaa ya kuonyesha mechi hiyo, hivyo kushindwa kufikiana makubaliano ya mechi hiyo kuonyeshwa moja kwa moja nchini Uingereza. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Nou Camp, Barclona na rais wa Laliga Javier Tebas amethibitisha hilo.

''Mchezo baina ya Barcelona na Real Madrid utachezwa siku ya Jumamosi majira ya saa 4:15 pm,'' Tebas aliiambia Cadena Ser. Hivyo mchezo huo hautaoneekana nchini Uingereza kwa sababu ya vikwazo kwenye televisheni kwa muda huo. 

Michezo yote ya ligi nchini Uingereza inaanza kutimua vumbi saa 16:00 CET au 15:00 GMT. FA kama msimamizi wa ligi hiyo siku zote hukabiliana na vyombo vya habari kuzuia kuonyesha mechi moja kwa moja kwa wakati huo wa saa kwa siku husika.   

Hii ni kutokana na kukabiliana na  hofu ya mahudhurio ya uwanjani, na kwa sababu hiyo mapato na picha za mchezo  yatapungua kama mchezo utaonyeshwa moja kwa moja kupitia kwenye runinga.  

Hivyo, Sky Sports ambao wanamiliki haki ya kuonyesha kila mchezo wa Laliga nchini Uingereza, kwa mara ya kwanza watashindwa kuonyesha mechi hiyo ya ''El-Clasico.   

Hiyo siyo mara ya kwanza kwa televisheni kushindwa kukubaliana juu ya matangazo yanayoleta utata nchini Uingereza kwani hata Kombe la FA mara nyingi wamekuwa wakilazimishwa kuonyesha marudio ya mechi kutokana na sheria za UEFA dhidi ya ratiba zake za mechi za Ligi ya Mabingwa.

No comments:

Post a Comment