Saturday, October 22, 2016

WACHINA WAMRUDISHA LIPPI ULINGONI.



Waswahili wanasema ng'ombe hazeeki maini na ndivyo ilivyotokea kwa kocha mkongwe Marcello Lippi kurudi tena kazini licha ya kustaafu kazi ya ukocha, baada y taifa la China kumpa kazi ya kuiona timu ya taifa baada ya mwenendo mbovu wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Russia.


Lippi na Bufon 2006 waliposhinda Kombe la Dunia.

Kocha huyo mkongwe aliyeshinda kombe la dunia mnamo mwaka 2006 na timu ya taifa ya Italia , amerudi katika soka baadaya kustaafau na sasa ndiye mkufunzi wa timu ya China, akimrithi Ngao Hongbo.
Lippi, mwenye umri wa miaka 68, alisimamia timu ya Italia mara mbili na kushinda matajai matano ya Serie A na taji la ubingwa barani Ulaya na timu ya Juventus.

Alistaafu ukufunzi baada ya kushinda taji la tatu mtawalai la ligi na timu ya Uchina Guangzhou Evergrande mnamo 2014.
China imeorodheshwa katika nafasi ya 84 duniani.
Gao Hongbo, alijiuzulu mapema mwezi huu baada ya kufungwa na Uzbekistan 2- 0 jambo linalodidimiza matumaini ya China kufuzu kwa kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

No comments:

Post a Comment