| Wachezaji wa Simba wakimpongeza Mavugo baada ya kufunga bao. |
Wakati jana watani wao Yanga wakishusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Kagera Sugar cha mabao 6-0, leo Mnyama ameendelea na rekodi yake ya kutopoteza baada ya kuifunga Toto Africans ya jijini Mwanza kwa bao 3-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa msimu huu na kuendelela kubaki kileleni mwa Ligi hiyo ya Vodacom Tanzania Bara.
Mabao ya Simba yalifungwa na Mzamiri dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza na ndani ya dakika ya 52 Mvugo aliyetokea benchi akaipatia Simba bao la pili kabla ya Mzamiru kuipatia Simba bao la tatu ndani ya dakika ya 74 na kuwafanya Simba kuondoka na pointi tatu muhimu.
Huko Sokoine nako Mbao FC walishindwa kuondoka na pointi tatu mbele ya Prisons baada ya kusawazisha bao ndani ya dakika ya 90 ya mchezo huo. Mbao ambao walikuwa wa kwanza kufunga ndani ya dakika ya 84 Boniface Maganga aliifungia Mbao bao lakini penati iliyopigwa na Lambert Sibianka wa Prisons iliwafanya Mbao kubakiza pointi tatu kwenye Uwanja wa Sokoine.
No comments:
Post a Comment