![]() |
| Messi akipongezwa na wachezaji wenzake. |
Penati ya lionel Messi ya dakika za majeruhi iliweza kuwafanya wababe wa Catalan kuondoka na pointi tatu kwenye Uwanja wa Mestalla Valencia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-2.
Ushindi haukuja kwa urahisi kwa Barcelona kwani walishuhudia kiungo wao Andre Iniesta akitolewa nje kwa kuumia goti na huenda atakuwa nje kwa muda mrefu.
Ingawa Barcelona walikuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao dakika ya 22 kupitia nyota wao Lionel Messi lakini ndani ya dakika ya 53 Valencia walisawazisha kupitia Munir kabla ya Rodrigo kufunga la pili kwa Valencia dakika ya 55, lakini alikuwa Luis Suarez aliebadili matokeo na kufanya 2-2 kwa bao lake la dakika ya 62 kabla ya Messi tena kufunga dakika ya 93 kwa penati. Na kuwafanya Barca kuondoka na pointi tatu ugenini. ![]() | |
| a Andre Iniesta akitolewa nje baada ya kuumia. |
Ushindi haukuja kwa urahisi kwa Barcelona kwani walishuhudia kiungo wao Andre Iniesta akitolewa nje kwa kuumia goti na huenda atakuwa nje kwa muda mrefu.


No comments:
Post a Comment