Ahmed Hossam Hussein ''Mido'', alizaliwa mnamo February 23 mwaka 1983 jijini Cairo Misri akicheza nafasi ya mshambuliaji alifahamika kwa utukutu wake na majivuno, akianza kazi yake ya uchezaji mpira mwaka 1999 na klabu ya Zamalek ya nchini Misri kabla ya kuijunga na Gent ya Ubeligiji mwaka 2000, ambako alishinda kiatu cha ''Belgian Ebony Shoe''.
Na baada ya hapo akaamia kwenye klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi mwaka 2001, na kutoka hapo akajiunga na Celta Vigo kwa mkopo mwaka 2003. Na baada ya hapo akatua Marseille ya nchini Ufaransa na kuachana nao mwaka 2004 na kutua Roma ya Italia, ambapo pia alichezea Tottenham Hotspur kwa mkopo kwa miezi 18 nwaka 2005 na akajiunga rasmi na klabu hiyo mwaka 2006. Lakinu akaachana na klabu hiyo na kujiunga na Middlesbrough, na alivyotoka hapo akajiunga na Wigan Athletic, Zamalek, West Ham United, na akarudi Ajax kwa mkopo.
Na mwaka 2011, akajiunga na Zamalek, kabla ya kujiunga na Barnsley mwaka 2012.
Mshambuliaji huyo ambaye alichezea timu ya taifa ya Misri mechi 51 na kufunga mabao 20 ambapo alichezea kuanzia mwaka 2011-2009.Alistaafu rasmi mpira June 2013. Na kukamilisha idadi ya mechi 221 na kufunga mabao 73 katika maisha yake ya soka. Kwasasa ni mshauri wa kiufundi kwenye klabu ya Lierse ambapo mwenyewe alisema kwamba uwepo wake klabuni hapo ni kwa ajili ya kuitangaza klabu hiyo kwenye Belgian First Division A. Pia ni mtangazaji wa televisheni.
No comments:
Post a Comment