Friday, October 28, 2016

MIAKA MITANO MBELE KILA MTU ATALIA JUU YA MESSI -MOURINHO.


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwamba miaka mitano mbele nyota machachari Lionel Messi atakuwa na miaka 34 na watu wote watalia juu yake, Mreno huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa anamuongelea kiungo wa Manchester United Michael Carrick kwanini anahitaji kupumzika zaidi kabla ya hapo awali ili kupunguza muda wake.
Carrick alikuwa nahodha kwenye mechi ya juzi ambapo dhidi ya Man City ambapo United walishinda 1-0 kwenye Kombe la EF, na akisistiza kuwa umri ndio sababu iliyomfanya kiungo huyo kukosa nafasi mara kwa mara kama misimu iliyopita.

''Ndani ya miaka mitano, hata Messi atakuwa na miaka 34  na wote tutalia juu yake, '' alisema Mourinho.Ni jambo moja kuwa na umri wa miaka 25 na mwingine 35, lakini ninachoweza kusema ni kwamba Carrick ni wa ajabu.

Mourinho ambaye ameonyesha kwamba ameridhika na Muingereza huyo ingwa hawezi kumtegemea zaidi Carrick kutokana na usawa wa dakika anazocheza.

''Siwezi kutarajia zaidi kutoka kwa Carrick kama ambavyo nitapata kutoka kwa Rashford au Herrera, katika suala la kucheza mechi tano mfulululizo,'' Mreno huyo alidokeza. Lakini yeye akiwapo uwanjani ni muhimu sana na anawapa wachezaji wengine uhuru wa kufikiria pale wanapohitaji.


Pia Mourinho alimzungumzia Mkhitaryan, ambaye nae hapewi nafasi nyingi za kucheza kama ilivyotarajiwa na Mourinho alimzungumzia mchezaji huyo kuwa ''Mkhitaryan anahitaji muda wa kuwa mchezaji bora na yeye anajua kuwa anaweza kuwa hivyo.'' Baadhi ya wachezaji wanahitaji muda zaidi wa kukabiliana na Premier League na majeruhi yake hayamsaidii kufanya msaada.

''Naamini kwamba mapema au baadaye hakutakuwa na matatizo yoyote na yeye atafikia malengo yake.''

No comments:

Post a Comment