Mchezaji mkongwe wa timu ya taifa ya Uholanzi Arjen Robben ameitwa kwenye kikosi cha Uholanzi kuwavaa Ubeligiji kwenye mechi ya kirafiki na mechi dhidi ya Luxembourg kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Winga huyo wa Bayern Munich ambaye ameshacheza mechi 88 kwa nchi yake, na mashindano sita makubwa toka alipoanza kulichezea taifa hilo mwaka 2003.
Robben ambaye toka November 2015 amekuwa na matatizo ya kuwa sawa kiafya kutokana na majeruhi ya hapa na pale. Na winga huyo mwenye miaka 32 tayali ameshafunga mabao sita kwa Bayern kwa msimu huu na pengine yamemshawishi meneja wa timu ya taifa Danny Blind kuweza kumuita tena kwenye kikosi chake kwenye mechi ya kundi A kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018.
Kikosi cha Uholanzi kilichoitwa ni pamoja-
Makipa-Maarten Stekelenburg (Everton), Michael Vorm (Tottenham).
Mabeki-Daley Blind (Man U), Jeffrey Bruma (Wolfsburg), Virgil Van Dijk (Southampton), Rick Karsdorp (Feyenoord), Terence Kongolo (Feyenoord), Joel Veltman (Ajax), JetroWillems (PSG).
Washambuliaji- Jordy Clasie (Southampton), Davy Klaassen (Ajax) Davy Propper (PSV), Bart Ramselaar (PSV), Stijn Schaars (Heerenveen), Wesley Sneijder (Galatasaray), Tonny Vilhena( Feyenoord), Georginio Wijnaldum (Liverpool).
Viungo- Memphis Depay (Man U), Bas Dost (Sporting), vicent Janssen (Tottenham), Luuk de Jong( PSV), Arjen Robben (Bayern Munich)

No comments:
Post a Comment