![]() |
| Mourinho na Klopp kocha wa Liverpool baada ya mechi kuisha.. |
Huenda kocha wa Mnchester United Jose Mourinho akapewa adhabu na FA baada ya matamshi aliyotaoa kwa mwamuzi Anthony Taylor aliyechezesha mechi baina ya Manchester united na Liverpool siku ya Jumatatu, kwenye uwanja wa Anfielde, pambano ambalo liliisha kwa sare ya 0-0 baina ya timu hizo mbili.
Na sasa Shirikisho la Soka England (FA)
limemwandikia barua Meneja wa Manchester United Jose Mourinho likimtaka
ajieleze kuhusu matamshi yake juu ya mwamuzi huyo. Na FA imempa Mourinho muda hadi Ijumaa kujielezea.
Uamuzi huo wa FA umekuja baada ya shirikisho hilo kuona amevunja Sheria kwa kuongea kuhusu waamuzi kabla ya mechi wanayopangiwa.
Mara
baada yamwamuzi Taylor, 37, kuteuliwa kuchezesha pambano hio
kuliibuka malalamiko, na hasa Mashabiki wa Liverpool, ambao walilivalia
njuga suala hilo kupitia kwenye Mitandao ya Kijamii.
Akiongea
na Wanahabari kabla ya Mechi hiyo, Mourinho aliulizwa kuhusu uteuzi wa
Refa huyo na yeye kujibu kwamba "Nadhani Bwana Taylor ni Refa mzuri
sana lakini anapewa presha kubwa na itakuwa ngumu kwake kuwa na kiwango
kizuri cha kuchezesha."
FA sasa inataka maelezo kutoka kwa
Mourinho kwa kuvunja Sheria iliyotungwa Mwaka 2009 inayokataza mameneja
kuongea lolote kuhusu marefa kabla ya Mechi.
Meneja wa kwanza
kabisa kuadhibiwa na Sheria hiyo alikuwa ni meneja wa zamani wa Man
United, Sir Alex Ferguson, ambaye alishitakiwa Mei 2011 kwa kutoa kauli
kuhusu Refa Howard Webb ambayo haikuwa mbaya bali ilikuwa ya kumsifia
pale aliposema alikuwa ni refa bora zaidi huko England.

No comments:
Post a Comment