Siku chache baada ya kuwa kwenye orodha ya kuwania tuzo ya Afrika, mwanasoka wa kimataifa wa Tanzania,
Mbwana Ally Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji amesema kwamba
kuingizwa kwenye kinyang'aniyo cha tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika ni
heshima kuu kwa nchi yake.
Samatta, amesema amefurahi sana juu ya uteuzi huo, kwani anajiona anaendelea kuiwakilisha vyema nchi yake katika soka.
Mwanasoka
Bora wa Afrika pamoja na kipa Mganda, Dennis Onyango anayechezea
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na kiungo Mkenya, Victor Wanyama
anayechezea Tottenham Hotspur ya England.
Orodha hiyo ina
Waalgeria watatu; mshambuliaji wa mabingwa wa England, Riyad Mahrez,
Islam Slimani wa Leicester City na El Arabi Hillel Soudani wa Dinamo
Zagreb
Mkongwe
Samuel Eto'o anayechezea Antalyaspor ya Uturuki naye yumo kwenye
orodha, pamoja na Mcameroon mwenzake, Benjamin Mounkandjo wa Lorient.
Wamo
pia Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Dortmund), Andre Ayew (Ghana na
West Ham), William Jebor (Liberia na Wydad Athletic Club), Mehdi
Benatia (Morocco na Juventus), Hakim Ziyech (Morocco na Ajax), John
Mikel Obi (Nigeria na Chelsea), Kelechi Iheanacho (Nigeria na Manchester
City).
Kuna pia Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal), Yannick
Bolasie (DRC na Everton), Sadio Mane (Senegal na Liverpool) na Kalidou
Koulibaly (Senegal na Napoli).
Samatta ndiye anashikilia tuzo ya
Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika aliyotwaa Januari mwaka huu kufuatia
kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe ya DRC mwaka jana
na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

No comments:
Post a Comment