Klabu ya soka ya Leicester City
imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani
Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Copenhagen.
Wakiwa
katika uwanja wao wa nyumbani King Power, Leicester walipata bao hilo
dakika tano kabla ya kwenda mapumzikoni kupitia kwa Riyad Mahrez
aliyekuwa katika kiwango cha hali ya juu baada ya kupokea pasi safi
kutoka kwa Mualgeria mwenzake Islam Slimani.
Kwa matokeo hayo Leicester wanabaki kileleni mwa kundi G wakiwa na
alama 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu ya ufnguzi wa ligi ya
mabingwa Ulaya.
Timu pekee zilizowahi kushinda michezo mitatu ya
ufunguzi katika michuano hiyo ni AC Milan, Paris St-Germain, Juventus na
Malaga.
kwa upande wa Juventus kipa wao mkongwe Gianluigi Buffon aliibuka shujaa kwa timu hiyo baada ya kuokoa penati ya Alexandra Lacazzete na kufanya idadi ya penati zilizookolewa kufikia nane kwa msimu huu wa klabu ya mabingwa Ulaya kati ya kumi na tatu. Na katika mchezo huo Juventus walishinda 1-0.
Matokeo mengine ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya
Bayer 04 Leverkusen 0-0 Tottenham Hotspur F.C.
CSKA Moscow 1-1 AS Monaco FC
Real Madrid 5-1 Legia Warsaw
Sporting 1 -2 Borussia Dortmund
Club Brugge 1-2 FC Porto
Dinamo Zagreb 0- 1 Sevilla
Leo kukiwa na michezo itakayoendelea na mkubwa zaidi ule wa Barcelona na Man City utakaopigwa NouCamp mchezo unaotazamiwa kuwa na upinzani mkali.

No comments:
Post a Comment