Thursday, October 20, 2016

MSN UTAIPENDA TU.

MSN, Messi, Suarez na Neymar.
Bila shaka hakuna shabiki, mdau au hata mchezaji asiyejua safu hatari ya washambuliaji iliyopo Barcelona maarufu kama MSN mchanganyiko wa Muargentina[Messi], Mbrazil[Neymar] na Mruguay[Suarez] safu hiyo ambayo inasemekana kuwa bora kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka imefikisha mabao 103 kwa mwaka huu 2016.
 Hat-trick ya jana kutoka kwa Lionel Messi na bao la Neymar kwenye Champions League dhidi ya Man City imeweza kusaidia safu hiyo kufikisha idadi hiyo kwenye soka kukiwa na miezi miwili tu mwaka huishe. 

Kurejea kwa Neymar kutoka kwenye michuano ya Olympic nchini Brazil na kuumia kwa Messi hakukufanya kuzuia mabao kutoka kwa safu hiyo, ambapo Messi toka arejee uwanjani ameshacheza na nyavu mara 4 sasa, huku Suarez akiwa na mabao 42 kwa mwaka huu huku Messi akiwa nyuma na mabao 40 na Neymar akiwa na 21. 

Huku tukitarajia kuona kama wataweza kuvunja rekodi yao ya mwaka 2015 ya mabao 137. Safu ya MSN inafanya kila liwezalo ili kuweka mambo sawa uwanjani.

No comments:

Post a Comment