Baada ya bundi wa sare kuikalia kooni klabu ya Yanga katika mechi zake zilizopita za hivi karibuni kwenye Ligi Kuu Bara, jana waliweza kuzinduka kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto Africans ya jijini Mwanza.
Ushindi huo unaifanya Yanga kupanda mpaka nafasi ya tatu kwenye
msimamo ikiwa na pointi 18 sawa na Kagera Sugar iliyo nafasi ya nne.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, timu hizo
zilikuwa zikishambuliana kwa zamu katika vipindi vyote viwili. Mabao ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 28 na dakika ya 55 Msuva alifunga bao la ushindi kwa mkwaju wa penati.
Yanga walipata penati hiyo baada ya Deus Kaseke kuangushwa eneo la hatari na Ramadhan Malima wa toto na mwamuzi Andrew Shamba wa Pwani alitoa penalti hiyo.
Simba inajivunia kwa kila kitu. Inaongoza kileleni kwa pointi 23 katika michezo tisa iliyocheza kati ya hiyo imeshinda saba, imepata sare mbili, ikiwa na jumla ya mabao ya kufunga 17 na kuruhusu kufungwa matatu pekee.
Kutoka kwenye uwanja wa hapo jana Uhuru Dar es Salaam, Majimaji ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji African Lyon.
Wafungaji wa Majimaji kwenye mechi hiyo walikuwa Peter Mapunda dakika
ya 64 na Marcel Bonaventure katika dakika ya 73. Kwa ushindi huo,
Majimaji imesogea kwa nafasi moja na sasa iko nafasi ya 15 ikiwa na
pointi tisa. Toto imeshuka mkiani ikiwa na pointi 8.
Katika mechi iliyochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, Ndanda
ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City huku Prisons ikishinda mabao
2-1 dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Prisons sasa imechupa mpaka nafasi ya sita ikiwa na pointi 15 na
Stand imebaki nafasi yake ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi zake
20. Nayo Ruvu Shooting ikiwa nyumbani kwenye uwanja Mabatini, ilitoka
sare ya bao 1-1 na Mwadui.

No comments:
Post a Comment