Licha ya kupoteza hapo jana dhidi ya timu yake ya zamani Barcelona, Meneja wa Manchester City Pepe
Guardiola amsema kuwa hatobadili filisofia yake licha ya klabu yake
kufungwa 4-0 na Barcelona katika uwanja wa Nou camp.
Lionel Messi
alifunga hat-trick dhidi ya Manchester City iliokuwa na safu ya ulinzi
ilio legea huku kipa Claudio Bravo akipewa kadi nyekundu kwa kushika
mpira nje ya eneo hatari.hakutakuwa na mabadiliko.
''Hadi siku ya mwisho ya kazi yangu kama mkufunzi nitajaribu kucheza kwa uwezo wetu'',alisema.
Barcelona inaongoza kundi C na pointi tisa ,ikiwa mbele kwa pointi tano.
City
ilikuwa nyuma kwa bao moja katika dakika za kwanza za kipindi cha pili
wakati Bravo aliposhika mpira na bahati mbaya ukamuangukia Luis Suarez.
Guardiola alisema kwamba mchezo ungekuwa wazi kama wangekuwa 11, ''tumepoteza 4-0 lakini sisi ni klabu mpya, tuanhitaji kujuana, ni klabu ambayo kwa miaka 35 ilikuwa nje ya Europe.''
''Tumekuja hapa kucheza na utu mkubwa lakini siku zote ni ngumu kucheza na Barcelona wakiwa 11 kwa 10 kwenye mchezo.

No comments:
Post a Comment