Friday, October 7, 2016

NEYMAR AFIKISHA MABAO 300.


Baada ya hapo jana kufungua kalamu ya mabao kwa timu yake ya taifa ya Brazili kwenye ushindi wao wa 5-0 dhidi ya Bolivia kwenye kuwania kufuzu Kombe la Dunia, mchezaji huyo mwenye miaka 24 ametimiza mabao 300 katika maisha yake ya soka.
Lilikuwa bao lake la 49 kwa taifa lake, huku akifunga 18 zaidi kwenye timu ya vijana ya Brazil pamoja na U-17 na U-20 upande wa Olimpiki. 

Na tangu ajiunge na Barcelona mpaka sasa ameshafunga mabao 95 na pamoja na yale ya klabu yake ya kwanza ya Santos mabao 138. 

No comments:

Post a Comment