![]() | |
Isco katika moja ya majukumu yake akiwa Real Madrid |
Timu ya Tottenham Hotspurs yenye makazi yake jijini London Uingereza imeonyesha nia ya kumtaka nyota wa Real Madrid Isco kwenye msimu wa dirisha dogo la usajili January mwakani.
Mchezaji huyo ambaye hapewi nafasi kwenye kikosi cha Madrid kumepelekea kocha wa klabu hiyo ya London Mauricio Pochettino kuonyesha nia ya kutaka kumsajili tena baada ya hapo awali kushindikana.
![]() |
Daniel Levy mwenyekiti wa Tottenham. |
Kutokana na Pochettino kuonyesha nia hiyo, mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy anafikiria kufanya jitihada ya kumsajili mchezaji huyo January, ili kuepuka ushindani wa kutaka sahihi yake kwa majira ya pili ya usajili.
Ingawa hapo awali Isco aliiambia MARCA kwamba anapenda kuendelea kubaki Santiago Bernabeu, lakini pia anaweza kuhamia sehemu nyingine iwapo hakutakuwepo mustakabali wa maisha yake ya baadaye klabuni hapo.
Ila inaonekana Los Blancos hawawezi kukubali ofa hiyo kutokana na Levy alivyowawekea ugumu klabu hiyo kwenye usajili wa Gareth Balle majira ya 2013.
No comments:
Post a Comment