Friday, October 7, 2016

ARGENTINA WATOA SARE NA PERU, HISPANIA IKISHINDWA KUTAMBA UGENINI.


Hapo jana kulikuwa na michezo iliyoendelea ya mataifa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, ambapo Argentina ilipata sare 2-2 dhidi ya Peru huku pengo la mshambuliaji wake Lionel Messi likionekana kwenye mchezo huo.
Nyota huyo wa Barcelona ambaye yuko nj'e akiuguza majeraha yake ya misuli aliyopata mwishoni mwa mwezi uliopita aliyopata kwenye mchezo wa Barcelona dhidi ya Atletico Madrid. 

Alikuwa beki wa Everton alifunga bao la kwanza kwa Argentina dakika ya 15 kipindi cha kwanza na Peru kipindi cha pili dakika ya 58 walisawazisha kupitia mchezaji wao Guerrerro huku Gonzalo Higuain akifunga bao la pili kwa Argentina dakika ya 77 lakini penati ya Cueva ndani ya dakika ya 85 ilizima ndoto za Albiceleste kuondoka na pointi tatu hapo jana.

Huko Italia nako, timu ya taifa hilo imeikomalia Hispania kwenye mchezo wao uliomalizika kwa sare ya 1-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Juventus turin. 



Hispania walikuwa wa kwanza kufunga bao hilo dakika ya 55 kupitia mchezaji wake Vitolo lakini penati ya dakika 82 ya De Rossi ilifanya mchezo huo kumalizika kwa sare. 
 

 

No comments:

Post a Comment