Saturday, October 29, 2016

RONALDO AFUNGA HAT-TRICK MADRID IKISHINDA 4-1.

Ronaldo akishangilia moja ya mabao yake.

Nyota wa Real Madrid Critiano Ronaldo ameweza kukata vilimilimi vya mashabiki waliokuwa wanambeza baada ya muada mrefu kuwa na ukame wa mabao ndani ya Los Blancos baada ya hii leo kufunga hat-trick kwenye ushindi wa Madrid wa 4-1 dhidi ya Deportivo Alaves. 


Mchezaji raia wa Brazil Deyverson alikuwa wa kwanza kuipatia bao Deportivo Alaves ndani ya dakika ya 7 kabla ya Madrid kupata penati iliyopigwa na Ronaldo dakika ya 16 na kufanya matokeo kuwa 1-1 kabla ya Ronaldo tena kufunga bao la pili kwa Madrid dakika ya 32 na Morata kufunga bao la tatu dakika ya 83 na kabla ya Ronaldo kukamilisha idadi ya ya mabao kwa bao lake la dakika ya 88 na kufanya Los Blancos kuondoka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Deportivo Alaves. Kwa matokeo hayo Madrid inaendelela kukaa kileleni mwa LaLiga.

No comments:

Post a Comment