Sunday, October 30, 2016

HIGUAIN AIUA NAPOLI JUVENTUS STADIUM.

Gonzalo higuain akipongezwa na wachezaji wenzake.

Ilikuwa mechi ambayo ilivuta hisia za watu wengi kwenye ligi ya  Serie A nchini Italia kati ya ''kibibi kizee cha Tarino'' Juventus na Napoli na hisia hizo zilikuwa juu ya mchezaji Gonzalo Higuain aliyekuwa akichezea Napoli kabla ya kujiunga na Juventus kwa uhamisho wa euro million 90. Uhamisho ambao ulimfanya Higuain aonekane kama msaliti kwa kujiunga na Juventus ambao ni wapinzani wa Napoli ambapo alifunga mabao 36 kwa msimu uliopita. Mchezo huo ulimalizika kwa Juve kushinda 2-1 dhidi ya Napoli kwenye Uwanja wa Juventus.
Katika mchezo huo Leonardo Bonucci alifunga bao la kuongoza kwa Juve dakika ya 55 kabla ya Callejon kusawazisha bao kwa Napoli dakika ya 54 na kufanya matokeo kuwa 1-1, lakini alikuwa Higuain aliyepeleka kilio kwa klabu yake hiyo ya zamani kwa bao lake la dakika ya 70 bao lililodumu mpaka dakika tisini za mchezo huo.

Ushindi huo unaifanya Juve kuongoza Ligi kwa tofauti ya pointi 5 dhidi ya Roma ambao wanashika nafasi ya pili huku Napoli wakiwa nafasi ya tatu. 

Mchezaji huyo alikumbana na kadhia ya jezi zake kutupwa kwenye mapipa ya takataka na kuchomwa moto pale alipokubali kujiunga na Juventus hali ambayo imepelekea kupewa usalama juu ya mashabiki wa Napoli , na hata kabla ya mechi meneja wa Napoli Maurizio Sarri alisema kwamba 'mshambuliaji huyo wa Argentina ''nitamsalimia kama baba ambaye mtoto wake amemkasirisha.''  Hali iliyopelekea Napoli kucheza bila mashabiki wake kwa sababu za kiusalama kwa Higuain ambaye ata alipofunga bao hilo akushangilia 

No comments:

Post a Comment