Klabu ya mtaa wa Msimbazi SIMBA SC leo itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa CCM Kambarage dhidi ya
Mwadui ikiwa ni mchezo wa pili kwa timu hiyo kucheza nje ya Dar es
Salaam baada ya ule dhidi ya Mbeya City, ambapo waliibuka na ushindi wa
mabao 2-0. . Mwadui ambayo iko nafasi ya tisa kimsimamo wiki iliyopita waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda.
Simba itakuwa kwenye Uwanja wa CC-M Kambarage, Shinyanga kukabiliana na timu ya Mwadui kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya soka ya
Tanzania Bara.
Simba ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu ligi hiyo ilipoanza Agosti mwaka huu,
ambapo tayari wameshacheza mechi 11, ikishinda mechi tisa na kutoka
sare mara mbili ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo. Kama Simba itaibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mwadui
ya Shinyanga, itazidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na
kujitengenezea mazingira mazuri ya kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza
kwa takribani miaka minne iliyopita.
Mchezo huo ambao unaonekana kuwa mgumu kwa timu zote mbili kwani Mwadui haijawahi kufungwa na Simba kwenye Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara na mchezo huo unachezwa nyumbani hivyo Simba watakuwa na kibarua kizito kuweza kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo. Huku kocha wa Simba Joseph Omog akisema mechi hiyo itakuwa ngumu kwani kwani
wapinzani wao wanatumia mabavu uwanjani, lakini watapambana ili
kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Omog alisema hana wasiwasi na kikosi
chake, kipo vizuri, akihofia ubaya wa viwanja vya mikoani ambavyo
alisema vinaweza kuwaathiri wachezaji wake, wasicheze kwa uhuru.
“Tumejiandaa vizuri kushinda, nimewaona wapinzani wetu ni wazuri,
lakini wanacheza soka la nguvu, hivyo wachezaji wangu wanatakiwa kuwa
tayari kukabiliana nao kwa aina ya soka.
Huku kocha msaidizi wa timu ya Mwadui, Khalid Adam alisema jana kuwa wamewasoma Simba
na wanajua wapi wawakamate, hivyo haitakuwa mechi rahisi kama mashabiki
wa Simba wanavyodhani kwamba wanakwenda kuchukuwa pointi tatu kwao na
kuondoka.
“Sidhani kama kuna sababu ya kuwahofia Simba, timu zote zinacheza kwa
kujituma kutokana na changamoto iliyopo ya ushindani wa msimu huu,
tunapeana maelekezo ya kuzingatia wawapo uwanjani wafanye nini kupata
ushindi, tulianza vibaya ila sasa tunakwenda vizuri,” alisema Khalid.
Mechi nyingine za leo zitakuwa ni; Mbeya City itaikaribisha Maji Maji
kwenye uwanja wa Sokoine, wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Ndanda
huku African Lyon ikiwakaribisha Prisons, Toto watakuwa wenyeji wa
Mtibwa Sugar.
No comments:
Post a Comment