Bundi bado anaizunguka Man City baada ya kuendelea kushindwa kupata ushindi kwenye mechi tano mfululizo. Hali inayofanya mambo yazidi kuwa magumu kwa Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola na kujikuta akishuhudia timu yake hiyo ikishindwa kupata ushindi katika mchezo wa tano mfululizo na mchezo wa tatu mfululizi katika Premier League.
Manchester City imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Southampton kwenye mchezo wa Premier League ulipoigwa leo kwenye Uwanja wa Etihad jijini Manchester.
Southampton walianza kupata bao kupitia kwa Nathan Redmond katika dakika ya 27 kisha City wakasawazisha katika dakika ya 55 kupitia kwa Kelechi Iheanacho.
No comments:
Post a Comment