![]() |
Pogba na Carrick wakishangilia bao. |
Mashetani wekundu Manchester United wamezinduka leo baada ya kuibamiza Swansea 3-1 kwenye mchezo wa Premier League leo hii, United ambao walipoteza mchezo wao dhidi ya Fenerbance kwenye Europa Ligi waliweza kujiimarisha na kufanikiwa kuondoka na ushindi huo kwenye Uwanja wa Liberty ambapo Paul Pogba alikuwa wa kwanza kufungua kapu la magoli ndani ya dakika ya 15 kabla ya IBrahimovic kufunga ndani ya dakika ya 21 na 33.
Huku Swansea wakipata bao kupitia mchezaji wao Hoorn dakika ya 69.
Kwa matokeo hayo yanaifanya United kusogea mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi hiyo.![]() |
Sadio Mane akifunga bao la kwanza. |
Nao Liverpool wameweza kuisambaratisha Watford kwa bao 6-1 mchezo wao na kuwafanya kukaa kileleni mwa Ligi hiyo, mabao ya Liver yaliwekwa kimiani na Sadio Mane dakika ya 27, Countinho dakika ya 30, Can 37, Firmino 57, Mane 60 na Wijnaldum 90 huku bao la kufutia machozi la Watford likifungwa na Janmaat dakika ya 75.
No comments:
Post a Comment