Monday, November 7, 2016

PACQUIAO ATAKA KUWAPA MASHABIKI MECHI YA MAYWEATHER.

Manny Paqcuiao akisherehekea ubingwa wa WBO.

Kama mashabiki na wapenzi wa mchezo wa boxing watataka kuona mchezo kati ya Floyd Mayweather Jr na bingwa wa WBO Manny Pacquiao basi yupo tayali kumkabili Mayweather kwa ridhaa ya mashabiki.
Baada ya Mfilipino huyo kurejea ulingoni kwa kishindo kwa kumpiga Jessie Vargas Las Vegas Jumamosi iliyopita, akaongelea kwa haraka juu ya mpambano wake na Mayweather.

Mara ya mwisho mabondia hao kukutana Mayweather aliibuka na ushindi dhidi ya Pacquiao mwaka jana, kabla ya wote wawili kustaafu mchezo wa ngumi.

Pacquiao ambaye mwezi Desemba anatimiza miaka 38, huku Mayweather akijiandaa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mwezi February akitarajia kutimiza miaka 40, lakini akiwa tayali keshalipiza kisasi kwa mbabe huyo.

''Sio kwa ajili yangu pekee, lakini kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi kama watataka mpambano huo kwanini usiwepo? Pacquiao aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumapili. ''Tunaweza kuliongelea hili kwa urahisi na sio tatizo.

''Sababu kwa sasa tunayo mawasiliano ya moja kwa moja na wao hivyo itakuwa rahisi kuongea nao juu ya hilo kama kutakuwa na mpambano.

''Ninaamini kama kutakuwa na mpambano au kama itatokea, nataka kuhakikishia mashabiki kwamba watapenda na nitawapa kila kitu kurudisha uaminifu wao kwangu.''

Pacquiao aliongezea ''Hatujafanya majadiliano kwa sasa, haliko kwenye mawazo yangu kwasasa juu ya mchezo ujao.

No comments:

Post a Comment