Sunday, November 6, 2016

TERRY AENDA MAPUMZIKO DUBAI AKIWA NA KITABU CHA SIR ALEX FERGUSON


Mkongwe, Kiongozi na Nahodha wa Chelsea John Terry yuko mapumzikoni nchini Dubai kuelekea mapumziko ya mechi za kimataifa, huku akitokea benchi kwenye mechi ambayo Chelsea walishinda 5-0 dhidi ya Everton usiku wa jana Jumamosi. 


Terry mwenye miaka 35 aliposti picha inayomuonyesha akiwa kwenye fukwe za hoteli ya Burj Al Arab akiwa amepumzika huku akiwa na kitabu cha aliyekuwa kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson kama ishara ya kwamba anatarajia kuwa kocha kwa hapo baadaye. 

Terry ambaye mashabiki wa Chelsea wanamtukuza kwa ubora wake kikosini hapo na klabu hapo aliposti picha zake za mapumziko akiwa na mkewe Toni kwenye mtandao wa Instagram.

Ukiwa mchezo wake wa kwanza Stamford Birdge toka alipoumia mwezi Septemba mwaka huu. huku akiwapongeza wachezaji wenzake waliosababisha ushindi huo.
 

No comments:

Post a Comment