Tuesday, November 1, 2016

MOURINHO AMRUDISHA SCHWEINSTEIGER KIKOSINI.


Mourinho na Bastian wakiwa mazoezini.
Kocha mtata wa Manchester United Jose Mourinho amemrudisha kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza cha Manchester United.
Kiungo huyo mwenye miaka 32 amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 23 tangu Jose Mourinho alipoteuliwa kuwa kocha msimu huu.


Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kwa mara ya mwisho aliichezea Man U mwezi Machi wakati Louis van Gaal alipokuwa kocha wa mashetani hao wekundu.

Alisema mwezi August kuwa hana tatizo binafsi na Mourinho na Man U itakuwa klabu yake ya mwisho kucheza barani Ulaya.
Huku mwenyewe alionyesha kufurahishwa na kurudi kwake kikosi cha kwanza. Huku wachezaji wenzake nao wakionyesha kufurahiswha na kurudi kwake.

Rooney akifurahia jambo na Schweinsteiger mazoezini.
''Ni vizuri kumuona amerejea tena ,'' alisema Luke Shaw. Tulipata taarifa siku chache zilizopita.

 ''Anaushwawishi mkubwa ndani ya vyumba vya kubadirishia nguo na uwanjani pia kwa wachezaji vijana kama sisi,'' aliongezea Shaw.

Lakini bado haijawekwa wazi kama Mourinho atamtumia Bastian kwenye kikosi chake cha kwanza.

No comments:

Post a Comment