Ni kama vile tuzo ya Fifa Ballon d'OR imekufa baada ya France Football kuchukua umiliki wake kwenye tuzo hiyo, lakini FIFA ina mpango mpya kwa ajili ya kuwazawadia wachezaji bora kwa mwaka 2016. FIFA ilitangaza Jumatatu mpango wake mpya wa tuzo ujulikanao kama BEST FIFA FOOTBALL AWARDS ambao utafuata mchakato mbalimbali wa kupiga kura ukiwa tofauti kama mfumo wa awali wa upigaji kura ambapo mfumo watakaoutumia kwasasa ni pamoja na kura za mashabiki ikiwemo pia kura kutoka kwa manodha wa timu za taifa pamoja na makocha ambao asilimia 50 itatoka kwao kwa ajili ya mchakato wa uteuzi na asilimia 50 nyingine kutoka kwenye vyombo vya habari na kura za mashabiki za mitandaoni. Ambapo kura zilizopita zilikuwa zinatoka kwa manahodha, makocha na waandishi wa habari tu.
Mchakato huo wa kupiga kura utaamua washindi katika makundi nane na utatolewa wiki hii.
The Best FIFA Men’s Player 2016
• The Best FIFA Women’s Player 2016
• The Best FIFA Men’s Coach 2016
• The Best FIFA Women’s Coach 2016
• The FIFA Puskás Award 2016
• The FIFA Fair Play Award 2016
• The FIFA Fan Award 2016
• FIFA FIFPro World XI
• The Best FIFA Women’s Player 2016
• The Best FIFA Men’s Coach 2016
• The Best FIFA Women’s Coach 2016
• The FIFA Puskás Award 2016
• The FIFA Fair Play Award 2016
• The FIFA Fan Award 2016
• FIFA FIFPro World XI
Mwezi Septemba gazeti la France Football lilitangaza kuchukua umiliki wa tuzo ya Ballon d'OR kama tuzo yake yenyewe tofauti na FIFA.
Na wiki iliyopita France Football walitoa mfumo wao mpya wa kura zitakavyopigwa. Tuzo hiyo ya heshima iliyoanzishwa mwaka 1956 kwa kutambua mchezaji bora wa katika Ulaya, na FIFA alijiunga 2010.
Lakini kabla ya FIFA Ballon d'OR kuundwa. FIFA alikuwa na tuzo yake mwenyewe iliyoitwa FIFA World Player Of The Year, tangui kuanzishwa tuzo ya wanawake kuanzishwa mwaka 2001 ambayo inaitwa FIFA WOMEN'S WORLD PLAYER na tuzo hizo zote mbili zitakuwepo lakini majina yatabadirika.
Na tuzo hizo zitafanyika jijini Zurich mwezi Januari mwakani. Nyota Lionell Messi na Cristiano Ronaldo wamekuwa wakipokezana tuzo kwa wakati huu na pengine mmoja wao huenda akaibuka mshindi wa ttuzo hiyo mpya kutoka FIFA.
No comments:
Post a Comment