Tuesday, November 1, 2016
MURRAY AKARIBIA KUWA BINGWA NAMBA 1 WA TENNIS.
Mcheza tenisi raia wa Uingereza Andy Murray anakaribia kuwa mcheza tenisi namba moja duniani wa mchezo huo kama atafanikiwa kushinda taji la Paris Masters ambapo bingwa namba moja wa mchezo huo Djokovic ameshindwa kutinga fainali.
Murray ambaye toka 2009 amekuwa mchezaji bora namba mbili wa mchezo huo anatrajia kutimiza ndoto yake ya kuwa namba 1 katika mchezo huo.
Djokovic na Murray wote wana umri wa miaka 29 wote walikuwa na maelfu ya pointi katika viwango vilivyotolewa mwezi Juni , lakini mshindi mara 12 wa Grand Slam Djokovic ameendelea kuwa na viwango bora na Murray ambaye lengo lake ni kuwa mchezaji wa pekee wa kiume kutoka Uingereza kuwa nafasi ya namba moja duniani..
''Nina stahili kuwa huko kwasababu namba haziongopi.''Alisema Murray.
''Tuna msimu mrefu. Tuna shughuli nyingi kwa muda mzuri kwa wachezai wote kucheza.
''Kama wewe ni namba moja,mbili au tatu jia kwamba wewe unastahili namba hiyo.
''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment