Sunday, September 18, 2016
KILIMANJARO QUEENS UTAIPENDA TU, YAIBAMIZA UGANDA 4-1 NA KUTINGA FAINALI
Timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania Bara ''Kilimanjaro Stars'' imeweza kutinga fainali baada ya kuifunga wenyeji Uganda 4-1 katika Michuano ya CECAFA kwa wanawake,mchezo uliochezwa katika uwanja wa FUFA Technical Center, Njeru. Magoli ya Donosia Daniel,Mwanahamisi Omari ,Stumai Abdalah ,na Asha Rashidi yaliweza kuisambaratisha Uganda na kuzima ndoto za wenyeji kucheza fainali ya michuano hiyo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika kwa wanawake.
Kilimanjaro Queens watakutana na Kenya ambao wamewafunga Ethiopia 3-2.Kesho mapumziko na Jumanne ndio Fainali yenyewe.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI KILIMANJARO QUEENS.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment