Wakati juzi Septemba 18 2016 mshambuliaji mahiri na hodari wa enzi ya miaka ya nyuma Ronaldo Nazario De Lima akitimiza miaka 40. Huku uzito mkubwa ukisitisha umahiri wake uwanjani lakini hilo bado halifuti rekodi zake nzuri alizopata kipindi anacheza soka maridadi na lililomvutia kila mtu kwa wakati huo.
Kwenye mwezi Desemba 1992 kocha wa Cristovao Roberto Gaglianone aliwaambia waandishi wa habari kuwa kijana huyo mwenye umri wa 16 ambaye ni mshambuliaji katika timu ya vijana ambae aliachana na timu hiyo na kujiunga na Cruzeiro kuwa anakwenda kuwa namba 9 inayofuata ya Brazil.
''Anakwenda kucheza Kombe la Dunia 1998,'' alieleza. Waliniuliza jina lake nami nikasema 'Ronaldo'. Lilikuwa ni jina ambalo litakuja kuwatisha mabeki na kila mtu. Hata kuweza kutokea kwa wengi.
Alesandra Nesta kila akirudia kutazama marudio ya Fainali UEFA ya Lazio waliopoteza kwa Inter Milan, kwa kukata tamaa na jitihada za kufanya kazi na kibaya alichofanya juu ya mwanasoka huyo usiku wa siku hiyo katika uwanja wa Parc des Princes, baada ya uwezo aliouonyesha Ronaldo katika goli alilofunga ambapo alipiga mpira uliomuacha nyuma kipa wa Biancocelesti Luca Marchegian asijue la kufanya.
Ronaldo na wachezaji wenzake waliweza kuwanyanyasa wakina Nesta na ujuzi wake hodari mwanzo wa kipindi hadi mwisho. Jambo ambalo Nesta kaja kuelezea kilichotokea baada ya kustaafu kwake.
''Uzoefu wangu mbaya katika maisha yangu ni siku niliyocheza dhidi ya Ronaldo na kupoteza 3-0 Paris lakini sasa sifikirii kuwa lilikuwa ni kosa langu,'' ameelezea. Ronaldo alikuwa hadhuiliki.
''Ni ngumu kutokubali kuwa wakati wa kilele chake, Ronaldo hakuwa mchezaji, alikuwa na mchanganyiko wa kipekee wa kasi, nguvu na uwezo wa kutoka mabeki. Hakuna aliewahi kutokea mwenye vitu kama yeye, kwani hakukuwa na wa kumkabili.'' Mchezaji wa zamani wa AC Milan Marcel Desailly alieleza.
''Ilikuwa kumuangalia yeye ni kama kumuangalia muhusika mkuu katika michezo ya video.''
''Alikuwa mchezaji halisi wa ''playstation game''.'' Mchezaji mwenzake wa Barcelona na ambae sasa hivi ni kocha wa timu hiyo Luis Enrique alisema. ''Sasa hivi tumezoea kumuona Messi akikokota wachezaji zaidi ya sita lakini sio tena.''
Sio jambo la kushangaza kama ukisikia kuwa Ronaldo ni chachu ya Messi kufanya vizuri. ''Alikuwa mshambuliaji ambaye sijapata kumuona.'' Na baadaye Messi alikiri kuwa ''Alikuwa na kasi na kuweza kufunga eneo lolote na kupiga mpira vizuri kuliko yeyote yule.''
''Nilicheza naye kipindi cha msimu wake mmoja akiwa Barcelona,'' Laurent Blac alielezea.
''Ilikuwa ni 1996-1997 na kwangu mimi ulikuwa mwaka mzuri kwake kwani Ronaldo alifunga magoli 47 katika mechi 49 za Barca na kushinda mataji matatu.
''Na baada ya hapo aliifunga kila timu kwa uwezo wake na kuwapita wachezaji kama vile hawakuwepo.''
''Nakumbuka goli moja ambalo alichukua mpira kutoka kwa kiungo na kukimbia nao huku nyuma wachezaji nane walikuwa wana mkimbiza. Ilikuwa ni uchizi na kutoamini nilichokuwa nakiona.''
''Ilikuwa kabla ya kuumia, na ninadhani baada ya hapo hakucheza kama yule tuliemzoea.''
Na ni kweli baada ya kuumia goti Ronaldo hakurudi katika hali yake kiuchezaji kama zamani, alipunguza kasi, maarifa na ujuzi kwa wapinzani wake.
No comments:
Post a Comment