Thursday, October 13, 2016

TOTTI ANAPASWA KUCHEZA MPAKA MIAKA 50 -MARADONA

Diego Maradona na Francensco Totti kwenye mechi ya hisani hapo jana.

Bingwa wa Kombe la Dunia 1986 Diego Maradona amewaambia AS Roma kwamba Francensco Totti anaweza kuendelea kucheza mpaka atakapofikisha miaka 50. Maradona alizungumza hayo kwenye mechi ya hisani jijini Rome Jumatano hii.
Maradona ameweka wazi kwamba angependa kumuona nyota huyo mwenye umri wa miaka 40 Totti akiendelea na kazi yake kwa miaka kumi zaidi. 

''Totti ni mzushi kwa kweli,'' alisema Maradona. 

''Anapaswa kucheza mpaka miaka 50. Nimemueleza Totti, ninakuomba usiachane na soka sababu ukifanya hilo nitachukia mpaka kifo. 

Kwa Serie A, Maradona anahisi klabu yake ya zamani ya Napoli inaweza kumaliza utawala wa Juventus.  

Amesema kwamba kama wataweza kucheza bila Arkadiusz Milik, ambaye yuko nje akiuguza majeraha ya goti, Napoli inaweza kushinda taji la ligi kuu, ingawa wako nyuma ya pointi nne kwa anaeongoza ligi.    

Maradona alisema, ''ukweli ni kuwa Napoli wanaweza kumfunga Juventus mwaka huu kama hawatafikiria kutokuwepo kwa Miliks zaidi. 

''Manolo Gabbiadini ataingia uwanjani akiwa na kujiamini zaidi na Napoli itashinda,'' 

No comments:

Post a Comment