Friday, September 16, 2016

BAYERN BILA MULLER,LAHM NA ALABA KUWAVAA INGOLSTADT, BUNDESLIGA WIKIENDI HII



Bayern Munich itaingia uwanjani wikiendi hii kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga dhidi ya Ingolstadt bila ya wachezaji wake watatu David Alaba, Thomas Muller na Philip Lahm kutokana na kuwa majeruhi. Lakini Arjen Robben na Jerome Boateng wakirejea uwanjani. 


Robben na Boateng wameendelea na mazoezi baada ya kuwa nj'e kutokana na majeruhi, lakini wote wako tayari kurejea uwanjani na wataanzia benchi jumamosi hii.     

''Alaba, Muller na Lahm hawatakuwepo kutokana na majeruhi. Robben na Boateng watakuwepo uwanjani na watakuwa benchi,'' Ancelotti aliwaambia News Conference.   


[Kingslay] Coman nae yuko fiti, na anafanya mazoezi vizuri na atacheza jumamosi hii nae Mats Hummers anaendelea vizuri na atacheza pia.  

''Tunahitaji kuwa makini ingawa kila mchezo unaweza kuwa mgumu kwetu. Ingolstadt wana kasi nyingi  na watajaribu kucheza soka la burudani na tunawapa 100% .'' 

''Nimetazama michezo yote ya Ingolstadt, kila timu ina uimara na udhaifu, tutajaribu kupata faida, ninatarajia mchezo wa wazi.'' Aliongeza Ancelotti. 

No comments:

Post a Comment