Wengine walikuwa na wikiendi nzuri huku wengine ikiwa mbaya.
Vijana wa Pep Guardiola wameendela kuchanua mbele ya Bournemonth, Arsenal wakiendelea na ushindi kwenye safari yao, Liverpool wakipeleka kipigo cha kwanza kwa vijana wa Conte na West Broam wakishinda 4.

Premier League imeendelea kuchukua sura mpya katika wiki za mwanzoni mwa msimu na tayali imeshaonyesha mtazamo tofauti kwa wafuasi wa Manchester City. Vijana wa Pep Guardiola walikuwa na kazi rahisi kwenye ushindi wao wa 4-0 dhidi ya Bournemouth kwenye uwanja wa Etihad, na kuwafanya kushinda mechi zao zote tano. Na kuwafanya kuongoza Ligi hiyo.
Everton wako nafasi pili, wakishinda mechi yao ya nne baada ya kuifunga 3-1Middlesbrough. Tottenham, Arsenal na Liverpool wakishinda huku mabingwa Leicester kupitia nyota wao Islam Silman akifunga mawili.
Hali haikuwa nzuri kwa upande wa Jose Mourinho na Man United baada ya kupoteza mechi yao ya tatu ndani ya siku nane.
1.Liverpool kurudi katika hali yao ya kutisha katika kushambulia.
Liver wanashambulia kutoka upande wowote. Mabeki na Viungo, Lovren (beki wa nyuma) na Henderson (kiungo wa kati) ambao wote wawili hao wametumia nguvu zao kuweza kuipa timu yao matokeo mazuri wikiendi iliyopita. Wamerudisha aina yao ya kushambulia.
2.Silman ameonyesha ahadi yake ya kwanza.
Mchezaji huyo aliesajiliwa na Leicester kwa kiasi cha Euro million 28 amefanya vizuri kwenye Champions League kwenye ushindi wa 3-1, na ameendelea kufungua akaunti yake kwenye Premier League kama ahadi yake kwa klabu hiyo. Mpaka sasa ameshafunga magoli 9 , ukijumlisha na saba kwenye klabu yake ya zamani ya Sporting Lisbon. Jorge Jesus amesema kuwa anaweza kufunga magoli 50 kama atapewa nafasi kama Jamie Vard, na hata kama hatofikisha idadi hiyo, itakuwa sawa kwani ameanza mwanzo mzuri.
3.Alex Iwobu ni mzuri katika maamuzi.
Iwobu ana vitu adimu kama mjomba yake Jay Jay Okocha, na alikuwa bora kwenye mchezo wao dhidi ya Hull City. Alikuwa na wakati bora na mzuri wa kucheza na Theo Walcott kwenye ushindi wa goli la pili siku ambayo ujanja wake na uhalisia wake pamoja na kasi yake ya kupeleka mashambulizi vilionekana. Kwa mchezji ambaye mara chache kuanza ni muhimu kuitumia nafasi hiyo kuonyesha uwezo wako kama ilivyokuwa kwa Iwobu.Kwani alionyesha uimara wa Arsenal kwa nafasi yake.
4.De Bruyne aendelea kunga'ra
Kwa hali ya sasa, Kevin De Bruyne anaweza kuwa mchezaji bora kwenye Premier League.
Mchezaji huyo alikuwa mwanaume wa mechi kwenye derby na Man United kwenye ushindi wa 2-1, kuonyesha kiwango dhidi ya Bournemouth kwa kufungua magoli kwenye mechi hiyo na kuongeza lingine.
Bila shaka hakuna mchezaji bora England kama yeye.
5.Nacer West Brom
Nacer Chadli alidhihirisha thamani yake ya Euro millioni 13 kwa Broms baada ya kuisadia timu hiyo kuisambaratisha West ham kwenye ushindi wa 4-2, magoli yake mawili yamemuweka kwenye nafasi nzuri klabuni hapo.
6.Toffees wanaweza kuwa kwenye nne bora
Gareth Barry akishangilia goli lake la 600 kweny Premier League
Koeman ni kocha bora ambaye yuko tofauti na Martinez, anaelewa umuhimu wa utofauti kati ya beki na mshambuliaji. Usije kushangaa akiipeleka Everton kwenye nafasi ya sita au ya nne msimu huu, sababu wako imara dhidi ya maadui wao.
7.Rooney matatizo bado yanamwandama
Rooney ameshindwa kufunga akiwa Vicaragua Road.
Ni kama vile Wayne Rooney halingani na thamani yake kwa upande wa Man United. Kwani kwenye mechi England na Slovakia alicheza vizuri sana na kujitahidi kila awezalo juu ya taifa lake.
Mourinho anakabiliwa na jukumu zito kama la kumtoa nahodha huyo. Pamoja na kupumzishwa kwenye safari ya Feyenood lakini hakuweza kufanya mazuri kwa timu yake ambayo ishapoteza mechi tatu.
8.Charlie Austin amethibitisha nafasi yake.
Austin akishanglia goli lake
Charlie Austin amethibitisha ubora wa nafasi yake kwenye mechi ambayo iliwafanya Southamption kushinda kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu dhidi ya Swansea. Austin ambaye alitolewa dhidi ya Sparta Prague katikati ya wik.Na alikuwa benchi kabla ya kuingia na kufunga goli hilo. Na pengine goli hilo linaweza kumshawishi Claude Puel katika kumuanzisha kwenye michezo mingine. Huku akisema kuwa ataongea na mastreka wake wote juu ya maamuzi na kutaka kuimarisha eneo la ulinzi.
9.Ni muda wa Stoke kuwa na hofu
Mark Hughes ameanza kupata jazba
Potteries walihitaji mechi saba kupata ushindi wao wa kwanza msimu uliopita Septemba 26 dhidi ya Bournemouth. Na kumaliza nafasi ya 19. Na sasa hii ni mechi yao ya tano katika Ligi baada ya moja kupata draw na kupoteza nne, Hali inayowafanya kuwapeleka kwenye kushuka daraja kama watakuwa na maendeleo mabaya ya namna hii, kushindwa kwao kuimalisha ulinzi pamija na kushambulia. Basi wanapaswa kupiga kengele ya hatari.
10.Sunderland wanahitaji kuendelea kuomba kwa ajili ya Defoe kuwa mzima.
Jermain Defoe alishindwa kuiokoa Sunderland peke yake baada ya kufungwa na Tottenham
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, aliweza kufunga magoli 18 na kuwaokoa Black Cats kushuka daraja msimu uliopita.
Defoe ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli mawili katika mechi nne za Ligi Kuu kwenye msimu huu kabla ya kupoteza katika uwanja wa White Lane, na ameendelea kuwapa tabu klabu yake ya zamani siku zote kila wanapokutana. Karibia awafanye Sunderland kuongoza kabla ya muda wa mapumziko.
Bila yeye, pengine itakuwa tabu kwa Sunderland.
No comments:
Post a Comment