Aliwahi kusema kuwa yuko kwenye pumzi zile zile za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, Antonie Griezmann anahitaji kuinua makombe makubwa kwa mujibu wake mwenyewe.
Kupoteza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na fainali ya michuano ya Ulaya, yote ikiwa dhidi ya kiungo wa Real Madrid na Ureno, Griezmann ameona kwamba kila akikaribia ushindi unapotea na kuambulia patupu.
''Kuwa miongoni mwa Messi na Ronaldo, nahitaji kuanza kushinda mataji zaidi,'' aliiambia L'Equipe.
''Kuongoza nafasi ya ushambuliaji kwa Atletico na timu ya taifa ya Ufaransa, Griezmann anakubali kwamba kuna ulazima wa kuendelea kufanya vizuri zaidi juu ya maendeleo yake.
''Mara kwa mara nina haja ya kuchukua majukumu zaidi katika mashambulizi'' aliongeza ''mimi ninatoa kila kitu katika uwanja na lazima kujifunza wakati wa kuwa na utulivu.''
Licha ya hilo kwa sasa Griezmann anaongoza kwenye ufungaji wa LaLiga na anaenda kwenye mechi ya Ufaransa dhidi ya Bulgaria kwenye kuwania kufuzu Kombe la Dunia huku akiwa katima mfumo wa moto mwekundu.
No comments:
Post a Comment