Monday, September 19, 2016

HAKUWA MZITO NI KAKA YANGU- ALISTAIR BROWNLEE



                                           Alistar kushoto akimsaidia Johhny kumaliza mbio hizo

Makaka wawili kutokea Uingereza wamesaidiana kumaliza mbio pamoja za World Triathlon nchini Mexico. Johnny Brownlee alisaidiwa na kaka yake kumaliza mbio hizo baada ya kuishiwa nguvu kutokana na hali hewa ya joto iliyokuwepo nchini Mexico. Alistar ambaye baadae alimwita ndugu yake huyo ''mpumbavu'' kwa kutokunywa maji ya kutosha.   

Zilibaki mita 700 kumaliza mbio hizo za mfululizo jijini Conzumel na Johhy alikuwa akiongoza mbio hizo, lakini kutokana na hali ya hewa ya joto alitaka kuishia njiani. 

                                 Jonny kulia akiendelea mbio hizo huku hali ya hewa ikimuumiza. 
Lilikuwa ni tukio lililowavutia mashabiki na watazamaji waliokuwepo uwanjani hapo.

                          Kaka hao wawili wakishangiliwa na mashabiki Cozumel

Alistar ambaye ni bingwa mara mbili wa Olimpiki ambaye hakuweza kumuona ndugu yake huyo akiishia njiani katika mbio hizo na kuamua kumpa msaada wa kukimbia nae na mpaka mwisho wa mstari wa kumaliza na kumuacha mdogo huyo kumaliza kabla yake.


                            Alistar akimsaidia Johhny kumaliza mbio hizo.

Ndugu hao walipitwa na Msouth Afrika Henri Schoeman na kushinda. 

Kama Jonny angeshinda mbio hizo za Mexico basi zingemfanya kukaribia taji la dunia. Huku Shirikisho la Hispania Triathlon lilikuwa linapinga ushindi huo kwa ndugu huyo lakini Shirikisho la Kimataifa la Triathlon liliunga mkono ushindi huo na kusema kuwa kwenye riadha kusaidiana kunaruhusiwa.  


                       Johhny akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuzimia kabla ya kupelekwa hospitali

Jonny ambae alizimia baada ya kumaliza mbio hizo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi, lakini baadaye aliposti picha mitandaoni na kuandika kuwa anaendelea vizuri na anamshukuru ndugu yake huyo kwa kumsaidia, huku akisema kuwa wameandika historia pamoja.   

Alistar ambaye nae alisema kwenye mahojiano yake kuwa ''katika hali ile ningemsaidia yoyote ambaye angekuwa karibu yangu na sio kwamba nimetoa msaada tu kwa mdogo wangu.    











 

No comments:

Post a Comment