Thursday, September 22, 2016

WATANI WA JADI LIGI KUU BARA VPL WAWINDANA KIMYA KIMYA.


Kuelekea Oktoba 1, ambapo lile pambano la kuwakutanisha mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya Vodacom  timu za Simba na Yanga likikaribia. Timu hizo ambazo ni mahasimu zinaendelea kutumia muda mwingi usiku na mchana kimya kimya kutengeneza mipango ya ushindi kuelekea mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Timu hizo ambazo zina vigogo wenye fedha ambapo mipango yao kila upande inafanya kimya kimya kuepuka kutoas faida kwa mwenzie, ingawa timu zote zina mechi moja kila mmoja kuelekea mchezo huo, lakini lengo kuu ni pointi 3 za Oktoba. 

Huku Mnyama akitaka kulipiza kisasi cha kufungwa mbili msimu uliopita, huku mahasimu wao Yanga wakisisitiza kutopoteza mchezo huo kwa mzunguko wa kwanza wa ligi. 

Simba iko kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 13, ikishinda mechi nne kati ya tano, huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 10, ikishinda mechi tatu kati ya nne.

Kocha wa Yanga Hans Pluijm, ambaye kikosi chake kitacheza na Stand United katika uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga, alisema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha hawapotezi mchezo wowote wa raundi ya kwanza , huku wakiwa na sare waliyoipata kwa Ndanda FC ya Mtwara.   

Akisisitiza kushinda mechi zao zote ikiwemo ile ya watani wao wa jadi, Simba mwanzoni mwa Oktoba.   

''Nimewaambia wachezaji wangu kuwa wasifikirie kutoka sare au kufungwa kwenye mechi zetu, Kila mchezo nataka watoke na pointi tatu. Huu ndiyo mkakati wangu,'' Alisema Pluijm.   

Aliongeza kwa kusema kuwa mechi zote ni ngumu kwetu msimu huu kwani kila timu imejipanga vizuri na sio kwamba mechi yao na Simba ndio ngumu.Aliongezea kocha huyo.

Kwa upande wa Simba, Joseph Omog amesema kuwa wamejiandaa vizuri na mchezo huo, lakini amesisitiza kuwa mechi yao dhidi ya Majimaji inaweza kuwa ngumu kuliko ya Yanga. 

''Kiufundi, mechi dhidi ya Majimaji inaweza kuwa ngumu kwa sababu wachezaji wa timu hiyo ya Songea hawafahamiki,'' alisema Omog. 

''Mchezo dhidi ya Yanga ni muhimu kwetu, lakini hatuwezi kuidharau mechi ya Majimaji na matokeo mazuri tatakayopata itakuwa tunaweka mkazo kwenye mechi ya Yanga.''

''Tunahitaji kushinda mechi zote bila kujali tunacheza na nani. Ubingwa ni mkusanyiko wa pointi nyingi za ushindi na siyo kutoka Yanga tu.''   



No comments:

Post a Comment